INVICTUS LAW & CONSULTANCTY

INVICTUS LAW & CONSULTANCY

Looking for a law firm that stands by your side with expertise and integrity?

You’ve come to the right place! Your first consultation is free and just one click away.

INVICTUS LAW & CONSULTANCY

Looking for a law firm that stands by your side with expertise and integrity?

You’ve come to the right place! Your first consultation is free and just one click away.

Professional Law Attorney

Built for the People We Serve

We started Invictus L & C with a simple belief: the law should work for people, not just the system. That means listening before advising, solving problems before quoting rules, and standing with you every step of the way.

Founder & Executive Partner

Professional Law Attorney

Built for the People We Serve

We started Invictus L & C with a simple belief: the law should work for people, not just the system. That means listening before advising, solving problems before quoting rules, and standing with you every step of the way.

Whether you’re making big moves or facing tough situations, we’re here to protect what matters most to you.

Founder & Executive Partner

What drives our Practice

We believe that exceptional legal outcomes are built on preparation, insight, and trust.
Our work begins long before we step into the courtroom—with strategic thinking, rigorous analysis, and a deep commitment to our clients.

Fields of Expertise

Practice Areas

Welcome to the heart of our expertise! Whether you’re dealing with the complexities of family law, starting a business, or defending your rights, we’re here to help you every step of the way. At Invictus L&C, we combine sharp legal skills with a touch of personal care to guide you through each challenge. Dive into our practice areas to discover how we can turn your legal challenges into stepping stones towards success.

LAND DISPUTES

_____________
Resolve land conflicts with expert advice, ensuring your property boundaries and ownership rights are clearly defined under Tanzanian law.

LAND DISPUTES

Protect your real estate interests with precise legal strategies that enforce your rights and bring lasting peace of mind.

MATRIMONIAL MATTERS

_____________
Receive expert guidance on divorce proceedings and child custody matters to ensure your family's interests are protected.

MATRIMONIAL MATTERS

Ensure fair resolution in marital disputes with dedicated legal support that protects your rights and the well-being of your family.

PROBATE AND ESTATE ADMINISTRATION

_____________
Navigate the complexities of probate and estate administration with expert guidance to ensure legal compliance and accuracy.

PROBATE AND ESTATE ADMINISTRATION

Simplify estate management and secure your legacy with precise legal support, ensuring your wishes are honored efficiently under Tanzanian law.

CRIMINAL DEFENSE

_____________
Receive robust defense against criminal charges, ensuring fair treatment and adherence to your rights under Tanzanian law.

CRIMINAL DEFENSE

Protect your freedom and future with strategic legal representation focused on achieving the best possible outcome in criminal proceedings.

LABOR AND EMPLOYMENT

_____________
Receive expert advice on navigating employment disputes, ensuring compliance with Tanzania’s labor laws to protect your rights as an employer or employee.

LABOR AND EMPLOYMENT

Resolve workplace issues effectively with legal strategies that safeguard your interests and promote a fair working environment.

BUSINESS INCORPORATION AND CONSULTATION

_____________
Receive professional guidance on business incorporation, ensuring your venture complies with Tanzanian corporate regulations and starts on a strong foundation.

BUSINESS INCORPORATION AND CONSULTATION

Optimize your business strategy and operations with expert consultation that positions your company for growth and success in Tanzania’s dynamic market.

Our Team

Meet Our Team

Monday 08:30 AM - 05:00 PM
Tuesday 08:30 AM - 05:00 PM
Wednesday 08:30 AM - 05:00 PM
Thursday 08:30 AM - 05:00 PM
Friday 08:30 AM - 05:00 PM
Saturday 09:30 AM - 01:00 PM
Sunday Closed

We're Here When You Need Us

Clarity starts with knowing when and how to reach your legal team. These are our working hours—set to ensure you’re never left wondering when to get in touch. We value your time, and we’re here to use it wisely.

Have a Legal Question or Need Assistance?

If you’re facing a legal issue or simply have a question about your rights or obligations, don’t hesitate to reach out. Whether it’s a dispute, a contract, or you’re unsure about a legal process—our team is ready to provide guidance and support. Fill out the form below and we’ll get back to you promptly.

Frequently Asked Questions

Masuala ya Ardhi na Umiliki wa Mali

  • Je, nawezaje kuzuia mtu asiingilie mipaka ya kiwanja changu?

    Kuingiliwa kwa mipaka ya kiwanja chako ni ukiukwaji wa haki yako ya miliki, na sheria ya Ardhi ya Tanzania inakupa njia kadhaa za kisheria kuzuia au kushughulikia hali hiyo. Hapa ni hatua unazoweza kuchukua:

    1. Thibitisha Mipaka Kisheria: Kabla ya kuchukua hatua dhidi ya mtu anayeingilia mipaka, hakikisha mipaka ya kiwanja chako inatambulika rasmi kupitia ramani ya upimaji (survey plan) au hati miliki. Hii ndiyo msingi wa kudai haki yako.
    2. Wasiliana Kijamii au Kiserikali: Jaribu kwanza njia ya kirafiki kwa kumweleza jirani kuhusu mipaka, kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa/kijiji au mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
    3. Toa Notisi ya Kisheria (Legal Notice): Ikiwa mtu ataendelea kuingilia, unaweza kupitia kwa wakili ambaye atatoa notisi ya kisheria (demand notice) kumtaka aondoke na kusitisha uvamizi au ujenzi.
    4. Fungua Kesi Baraza la Ardhi au Mahakama: Ikiwa uvamizi utaendelea licha ya onyo, unaweza kufungua shauri katika Baraza la Ardhi la Kata au mahakama, ukiomba amri ya zuio (injunction) na hata kuamriwa aondoke.
    5. Omba Hatua ya Kitaaluma ya Upimaji: Unaweza kuomba kupimiwa mipaka upya na ofisa ardhi wa halmashauri ili kuthibitisha mipaka, hasa kama jirani anapinga ramani yako. Hili husaidia kuondoa utata wa eneo husika.
    6. Zuia Ujenzi kwa Notisi ya Mahakama: Ikiwa mtu anajenga ndani ya kiwanja chako, unaweza kuomba temporary injunction kutoka mahakamani ili asiendelee na ujenzi hadi shauri litakapoamuliwa.

    Angalizo: Usichukue sheria mkononi kama kubomoa jengo au kumfukuza mtu kwa nguvu. Hii inaweza kukufanya nawe ukaonekana mkosaji mbele ya sheria.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia kuthibitisha mipaka yako, kutoa notisi za kisheria, kufungua mashauri, na kukulinda dhidi ya uvamizi wa aina yoyote. Tunasimamia haki zako kwa nguvu ya sheria.

  • Haki zangu ni zipi kama mnunuzi wa ardhi iliyopo kwenye mgogoro?

    Kununua ardhi yenye mgogoro ni jambo lenye changamoto kubwa kisheria. Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, haki zako kama mnunuzi wa ardhi inayogombaniwa zinategemea uhalali wa mchakato wa ununuzi na ujuzi wako kuhusu mgogoro huo kabla ya kununua.

    Haki zako kuu ni hizi:

    1. Haki ya Kulindwa kama Mnunuzi wa Nia Njema (Bona Fide Purchaser): Ikiwa ulinunua bila kufahamu kuwa kuna mgogoro na ukafuata taratibu zote za kisheria, unaweza kulindwa na mahakama kama mnunuzi wa nia njema. Lakini, hii ni kwa sharti kuwa haukuwa na taarifa yoyote kuhusu mgogoro huo kabla ya manunuzi.
    2. Haki ya Kurejeshewa Fedha (Rescission & Refund): Endapo itaonekana kuwa uuzaji haukuwa halali kutokana na mgogoro uliokuwepo, unaweza kuwa na haki ya kurejeshewa fedha zako na muuzaji kupitia njia ya madai mahakamani au kupitia usuluhishi.
    3. Haki ya Kufungua Kesi Mahakamani: Unaweza kufungua kesi mahakamani kudai uhalali wa umiliki wako, hasa kama una mkataba halali na ushahidi kuwa ulifuata taratibu. Mahakama inaweza kutoa amri ya kutambua umiliki wako au kulazimisha pande nyingine kukamilisha uhamisho wa ardhi.
    4. Haki ya Kufungua Pingamizi kwa Hati au Mchakato wa Usajili: Ikiwa mgogoro unahusiana na hati ya umiliki, unaweza kuwasilisha pingamizi rasmi kwa Kamishna wa Ardhi au kwa Baraza la Ardhi ili kusimamisha au kupinga usajili unaoendelea.
    5. Haki ya Kufuta Mkataba wa Mauziano kwa Udanganyifu: Iwapo muuzaji alificha taarifa kuhusu mgogoro kwa makusudi, unaweza kufuta mkataba kwa sababu ya udanganyifu (fraud) na kudai fidia.

    Angalizo: Sheria ya Ardhi na kanuni zake zinasisitiza kwamba mnunuzi ana wajibu wa kuchunguza ("caveat emptor") kabla ya kununua. Ikiwa ulijua kuwa kuna mgogoro lakini ukaendelea kununua, unaweza kupoteza haki fulani za msingi.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia kuchunguza historia ya ardhi, kufuatilia migogoro iliyopo, na kukushauri hatua sahihi za kuchukua kabla au baada ya manunuzi. Tunakutetea kwa weledi ili uweze kulinda haki zako kwa usalama wa kisheria.

  • Ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kununua kiwanja ambacho hakijapimwa?

    Kununua kiwanja ambacho hakijapimwa (ambacho hakijawekewa mipaka rasmi na serikali) kunaweza kuwa na faida ya bei nafuu, lakini pia kuna hatari nyingi za kisheria. Haya ni mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanya uamuzi:

    1. Thibitisha Umiliki Halali: Hakikisha muuzaji ni mmiliki halali wa kiwanja. Tafuta nyaraka za umiliki wa kimila, mikataba ya awali ya mauziano, barua ya serikali ya kijiji/mtaa, au uthibitisho wa kurithi ikiwa ardhi ni ya familia.
    2. Ushiriki wa Serikali ya Mtaa/Kijiji: Wasiliana na uongozi wa eneo husika kuthibitisha kuwa ardhi hiyo haijauzwa mara mbili, haiko kwenye mgogoro, wala si ya hifadhi ya serikali.
    3. Angalia Migogoro Iliyopo au Yaweza Kutokea: Fanya uchunguzi binafsi au wa kisheria kuhakikisha hakuna madai ya ndugu, majirani au mtu mwingine yeyote kuhusu kiwanja hicho.
    4. Tengeneza Mkataba wa Mauziano: Mkataba huu uwe wa maandishi, uwe na mashahidi, na uthibitishwe na mamlaka ya eneo husika. Hii itakusaidia katika hatua za baadaye za usajili.
    5. Omba Kupimiwa Rasmi (Survey): Baada ya kununua, chukua hatua ya kuwasiliana na ofisi ya ardhi ya wilaya ili kupimiwa rasmi na kuomba hati miliki. Hii itakupa ulinzi kamili wa kisheria.
    6. Epuka makubaliano ya mdomo: Usifanye makubaliano ama miamala ya ardhi kwa kuamini tu makubaliano ya mdomo. Yafanye yote kisheria na kwa maandishi. 

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia katika ukaguzi wa umiliki, uandaaji wa mikataba ya mauziano, na taratibu za kupimiwa kiwanja hadi upate hati miliki. Tunahakikisha unafanya uwekezaji salama na halali kisheria.

  • Je, ninaweza kuuza ardhi ambayo haijasajiliwa?

    Kisheria, unaweza kuuza ardhi ambayo haijasajiliwa, lakini kuna masharti na tahadhari muhimu zinazopaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha uuzaji huo ni halali na unalindwa kisheria:

    1. Aina ya Umiliki: Ardhi nyingi zisizosajiliwa ni zile zinazoangukia katika mfumo wa umiliki wa kimila, hasa vijijini. Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 (The Village Land Act na The Land Act) inatambua umiliki wa kimila, lakini inashauri usajili kufanyika kwa usalama wa miamala.
    2. Makubaliano ya Kimaandishi: Hata kama ardhi haijasajiliwa, mkataba wa mauziano unapaswa kuwepo kwa maandishi na uwe na mashahidi. Pia, ni vyema mkataba huo uthibitishwe na mamlaka husika kama serikali ya kijiji au mtaa.
    3. Idhini ya Serikali ya Kijiji/Mtaa: Kwa ardhi ya kimila, uhamisho wa umiliki unahitaji idhini ya serikali ya kijiji. Kukosekana kwa idhini hiyo kunaweza kufanya uuzaji huo kuwa batili au kuwekewa pingamizi baadaye.
    4. Hatari za Kisheria: Kukosa hati miliki (Certificate of Title) kunamaanisha kuwa mnunuzi hatakuwa na kinga kamili ya kisheria dhidi ya mtu mwingine anayedai umiliki. Hii inaweza kusababisha migogoro ya baadaye.
    5. Ushauri wa Kisheria: Kabla ya kuuza ardhi isiyosajiliwa, ni busara kushauriana na wakili ili kuhakikisha kuwa hatua zote muhimu zimefuatwa, na mnunuzi anafahamu hali halisi ya umiliki.

    Kwa hivyo, jibu fupi ni “Ndiyo, unaweza,” lakini ni jambo linalohitaji uangalifu mkubwa wa kisheria.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia kuandaa mikataba halali, kuhakikisha taratibu zote zimezingatiwa, na kukuongoza katika usajili wa ardhi ili biashara yako iwe salama na halali kisheria.

  • Je, ni hatua gani zichukuliwe pale mtu anapovamia kiwanja changu?


    Kuvamiwa kwa kiwanja ni hali inayoweza kuathiri haki yako ya kisheria na matumizi ya ardhi. Unapaswa kuchukua hatua zifuatazo kulinda umiliki wako halali:

    1. Kukusanya Ushahidi wa Umiliki: Hakikisha una nyaraka halali kama hati miliki, hati ya kimila, mkataba wa mauziano, au vielelezo vingine vya umiliki. Pia weka kumbukumbu ya uvamizi kwa picha, video au mashahidi.
    2. Kutoa Taarifa kwa Serikali ya Mtaa au Kijiji: Ripoti tukio hilo kwa uongozi wa mtaa au kijiji husika. Mara nyingi, viongozi hawa wanaweza kuanzisha majadiliano ya awali au kutoa taarifa ya msingi itakayosaidia hatua za kisheria.
    3. Kutoa Notisi ya Kuondoka (Eviction Notice): Unaweza kumpatia mvamizi notisi rasmi ya kisheria kumtaka kuondoka ndani ya muda maalum. Notisi hii inaweza kutolewa na wewe au kupitia kwa wakili wako, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuonyesha kutokukubaliana na uvamizi.
    4. Kufungua Kesi Mahakamani: Iwapo mvamizi hatatii notisi, unaweza kufungua kesi katika mahakama husika (ya Mwanzo, ya Wilaya au Baraza la Ardhi) ukiomba fatuatayo:
    • Amri ya kuondolewa kwa mvamizi (eviction order)
    • Fidia kwa usumbufu au uharibifu
    • Amri ya kuthibitishwa kuwa wewe ndiye mmiliki halali (declaratory order)

    6. Kuwasilisha Pingamizi kwa Kamishna wa Ardhi: Endapo mvamizi amefanikisha kupata hati miliki kwa njia ya udanganyifu, unaweza kuwasilisha pingamizi rasmi kwa Kamishna wa Ardhi ili kupinga uhalali wa usajili huo. Unaweza pia kufungua kesi ya kufuta hati hiyo kupitia Baraza la Ardhi ya Ardhi.

    7. Epuka Kujichukulia Sheria Mkononi: Kamwe usijaribu kutumia nguvu binafsi kumtoa mvamizi, kwani hatua hiyo inaweza kukufanya ushutumiwe kwa kuvunja sheria. Fuata taratibu za kisheria ambazo zinakulinda kikamilifu.

    Katika masuala nyeti kama haya ya migogoro ya ardhi, usisite kuwasiliana nasi Invictus Law and Consultancy. Tunatoa msaada wa haraka, ushauri wa kitaalamu, na uwakilishi wa kisheria ili kuhakikisha haki yako inalindwa kikamilifu na kisheria.

  • Je, ninawezaje kuthibitisha umiliki halali wa ardhi?

    Ili kuthibitisha umiliki halali wa ardhi nchini Tanzania, ni muhimu kuwa na vielelezo vya kisheria vinavyotambuliwa na mamlaka husika. Umiliki halali unaweza kuthibitishwa kwa kutumia nyaraka zifuatazo, kutegemea aina ya ardhi na mfumo wa usajili:

    1. Hati ya Hakimiliki (Certificate of Title): Hii ni nyaraka kuu inayotolewa na Wizara ya Ardhi kupitia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, ikiwa na jina la mmiliki, ukubwa wa eneo, matumizi yaliyokusudiwa, na muda wa umiliki. Hii ni ushahidi mkuu wa umiliki wa ardhi ya mjini au inayosajiliwa kisheria.
    2. Hati ya Kimila (Customary Right of Occupancy): Kwa maeneo ya vijijini, mtu anaweza kuthibitisha umiliki wake kwa hati ya kimila inayotolewa na Halmashauri ya Kijiji au Wilaya kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji (Village Land Act, Sura ya 114).
    3. Risiti za manunuzi na mikataba ya mauzo ya ardhi: Ingawa hazitoshi peke yake kuthibitisha umiliki halali, nyaraka hizi ni muhimu kuonesha historia ya umiliki. Zinapaswa kuambatana na ushahidi wa kuhamishiwa kwa haki ya umiliki kupitia taratibu halali kama vile usajili wa mkataba.
    4. Barua ya umiliki kutoka kwa serikali ya mtaa au kijiji: Hii hutumika mara nyingi kama uthibitisho wa muda au nyongeza ya nyaraka nyingine, hasa katika maeneo ambayo hayajasajiliwa rasmi.
    5. Ushahidi wa matumizi ya ardhi kwa muda mrefu (adverse possession): Katika baadhi ya mazingira ya kisheria, mtu anaweza kudai umiliki wa ardhi ikiwa ameitumia bila kupingwa kwa muda mrefu (takribani miaka 12 au zaidi), lakini hili huhitaji uamuzi wa mahakama.

    Tahadhari Muhimu:

    Umiliki wa ardhi unapaswa kuthibitishwa na usajili rasmi. Kumiliki ardhi bila hati kunamweka mtu katika hatari ya migogoro au kunyang’anywa. Aidha, hati miliki inaweza kuhakikiwa katika Ofisi ya Ardhi ya Wilaya au Kanda au kwa kutumia mfumo wa ardhi wa kielektroniki (Integrated Land Management Information System - ILMIS) unaoendeshwa na serikali.

    Kwa usaidizi wa kisheria katika uhakiki wa hati, usuluhishi wa migogoro ya ardhi, au uandikishaji wa umiliki wa ardhi, wasiliana nasi Invictus Law and Consultancy. Timu yetu ya wanasheria ina uzoefu mkubwa wa kushughulikia masuala ya ardhi kwa weledi, kasi na uaminifu.

Masuala ya Urithi na Mirathi

  • Wosia ni nini na unaandikwaje ili utambulike kisheria?

    Wosia ni tamko rasmi la maandishi au la mdomo ambalo mtu huweka mapema kabla ya kifo chake, akieleza jinsi anavyotaka mali zake kugawiwa baada ya kufariki dunia. Wosia husaidia kuondoa migogoro ya kifamilia na kuhakikisha mali zinagawiwa kulingana na mapenzi ya marehemu.

    Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hasa Sheria ya Mirathi ya Kiraia (Probate and Administration of Estates Act), ili wosia utambulike kisheria ni lazima uzingatie masharti yafuatayo:

    1. Awe na Akili Timamu:

    Muandishi wa wosia (testator) lazima awe mtu mzima (mwenye umri wa miaka 18 au zaidi) na mwenye akili timamu wakati wa kuandika wosia.

    2. Awe na Hiari:

    Wosia lazima uandikwe kwa hiari bila kushinikizwa au kulazimishwa na mtu yeyote.

    3. Maandishi na Sahihi:

    Wosia wa maandishi lazima uandikwe kwa maandishi, usainiwe na muandishi wake mbele ya mashahidi wasiopungua wawili. Mashahidi hao nao lazima wasaini mbele ya muandishi na mbele ya kila mmoja wao.

    4. Uainishaji wa Mali:

    Lazima wosia uonyeshe kwa uwazi aina ya mali inayogawiwa na jina au utambulisho wa kila mnufaika.

    5. Uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi:

    Wosia unaweza kumtaja mtu atakayesimamia utekelezaji wa wosia huo baada ya kifo cha muandishi (anayejulikana kama msimamizi wa mirathi au executor).

    6. Uhalali wa Kisheria:

    Wosia hauwezi kuondoa haki za kisheria za baadhi ya watu kama wake au watoto wa marehemu kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuwaacha bila kitu, isipokuwa kwa sababu maalum na halali.

    Tahadhari: Wosia wa mdomo unatambulika tu katika mazingira maalum, kama vile hali ya dharura, na lazima uthibitishwe na mashahidi wasiopungua wawili waliohudhuria tamko hilo. Pia, unakoma kutambulika baada ya siku 30 kama muhusika hakufariki.

    Invictus Law and Consultancy tunatoa huduma ya ushauri na uandishi wa wosia unaozingatia misingi ya kisheria ili kuhakikisha mapenzi yako yanasimamiwa ipasavyo bila kuacha migogoro kwa familia yako. Wasiliana nasi ili tukusaidie kuandika wosia salama, halali, na unaotambulika kisheria.

  • Je, ndugu wanaweza kuninyima urithi wa mzazi wangu?

    Kisheria, ndugu hawawezi kukunyima haki yako ya kurithi mali ya mzazi wako iwapo wewe ni mrithi halali kwa mujibu wa sheria, mila au dini inayotumika. Haki ya kurithi hutegemea mfumo unaotumika katika familia husika, ambao unaweza kuwa:

    1. Sheria ya Kimila: Ikitumika, mirathi hugawanywa kulingana na mila za kabila husika. Hata hivyo, mila hizo hazipaswi kukiuka haki za msingi, hasa za wanawake na watoto, kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zingine za nchi.
    2. Sheria ya Kiserikali (Statutory Law): Sheria kama vile Sheria ya Mirathi ya Kiraia (Probate and Administration of Estates Act) huweka utaratibu wa kugawa mali kwa warithi wote kwa haki sawa au kwa uwiano unaoelezwa kisheria. Hii husaidia hasa pale ambapo hakuna wosia.
    3. Sheria ya Kidini (Kiislamu/Kikristo): Ikitumika, mali hugawiwa kulingana na misingi ya dini hiyo. Kwa mfano, katika sheria ya Kiislamu, idadi ya sehemu za urithi hugawanywa kwa mujibu wa mafundisho ya dini.
    • Ikiwa ndugu wanajaribu kukunyima haki yako ya urithi kwa njia isiyo ya kisheria, unaweza:
    • Kufungua kesi ya mirathi mahakamani.
    • Kuweka pingamizi kwenye mchakato wa kugawa mali iwapo unaendelea bila haki.
    • Kuweka pingamizi kwenye wosia kama unaamini umeandaliwa kwa hila au bila kuzingatia sheria.

    Kumbuka: Mchakato wa urithi haupaswi kufanywa kwa nguvu au hila. Ni haki yako kudai sehemu yako ya urithi na mahakama inaweza kuingilia iwapo kuna ukiukwaji wa sheria.

    Invictus Law and Consultancy tumejikita katika kuhakikisha haki za warithi zinalindwa ipasavyo. Kama unakabiliwa na mgogoro wa urithi, usisite kuwasiliana nasi ili tukushauri na kukuwakilisha kwa ufanisi.

  • Je, ni hatua gani za kufungua mirathi mahakamani?

    Fungua mirathi mahakamani ni utaratibu wa kisheria wa kurasimisha usimamizi na mgawanyo wa mali za marehemu. Iwapo mtu amefariki dunia akiwa na mali, na anahitajika mtu kusimamia au kugawa mali hizo, hatua zifuatazo zinapaswa kufuatwa:

    Tafuta Cheti cha Kifo: Hiki ni nyaraka ya msingi inayoonesha kuwa mtu fulani amefariki. Inatolewa na ofisi ya serikali ya mtaa au hospitali aliyofariki marehemu.

    Tambua Aina ya Mahakama: Ikiwa marehemu aliacha wosia, kesi hufunguliwa kama Probate of Will katika Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi.

    Ikiwa hakukuwa na wosia, kesi hufunguliwa kama Letters of Administration katika Mahakama ya Mwanzo au ya juu kulingana na thamani ya mali.

    Tayarisha Hati Muhimu za Kesi:

    • Kwa kawaida, utahitaji:
    • Maombi rasmi (petition)
    • Orodha ya warithi
    • Orodha ya mali za marehemu
    • Kiapo cha usimamizi wa mirathi (affidavit of administrator)
    • Barua ya kuunga mkono kutoka kwa ndugu au warithi (consent)

    Wasilisha Mahakamani: Maombi hayo hupelekwa mahakamani ambapo yatapitiwa, na mahakama itatoa Matangazo ya Umma kwa kipindi cha siku 90 ili kuruhusu mtu yeyote mwenye pingamizi ajitokeze.

    Kusikilizwa kwa Maombi: Endapo hakuna pingamizi, mahakama itasikiliza maombi na kumpa mwombaji barua rasmi za usimamizi wa mirathi (Grant of Letters of Administration au Probate kama kuna wosia).

    Kutekeleza Majukumu ya Usimamizi: Msimamizi aliyeteuliwa atahitajika kuandaa taarifa ya mali, kulipa madeni ya marehemu, na hatimaye kugawa mali kwa warithi kwa kufuata sheria au maelekezo ya wosia.

    Tahadhari: Kutoa taarifa ya uongo au kuficha mali ya marehemu kunaweza kusababisha kesi ya jinai au kufutiwa mamlaka ya usimamizi.

    Invictus Law and Consultancy tunakusaidia katika hatua zote za kufungua na kusimamia mirathi kwa njia salama, ya kisheria na isiyo na usumbufu. Wasiliana nasi tukusaidie kulinda haki zako na kuhakikisha familia haingii kwenye migogoro ya urithi.

  • Nifanyeje ili kurithisha mali zangu kwa watoto wangu kisheria?


    Ikiwa ungetamani kuona watoto wako wakiwa salama na wakiendelea kunufaika na mali zako hata baada ya wewe kutokuwa nao karibu, ni busara kupanga urithi wako mapema kwa njia halali. Hatua muhimu za kufuata ni hizi:

    1. Andaa Wosia (Will):Hii ndiyo njia bora na rahisi ya kuelekeza ni nani atanufaika na mali zako. Wosia huandikwa kwa maandishi na kusainiwa mbele ya mashahidi wasiopungua wawili. Ndani yake, unaeleza wazi ni mtoto gani atapata nini.
    2. Hifadhi Wosia kwa Usalama: Wosia unaweza kuhifadhiwa nyumbani kwa mtu unayemuamini, au kuwasilishwa katika ofisi ya Msajili wa Wosia au mahakamani ili uwe salama na upatikane kwa wakati unaofaa.
    3. Thibitisha Umiliki wa Mali: Hakikisha mali unazotaka kurithisha zina hati au nyaraka halali zilizosajiliwa kwa jina lako. Ikiwa ni kiwanja, hati miliki ya ardhi iwepo; ikiwa ni akaunti benki, jina lako lionekane.
    4. Fikiria Zawadi ya Maisha: Unaweza pia kuanza kuwapatia watoto baadhi ya mali ukiwa hai, kupitia makubaliano ya kisheria yanayothibitisha uhamisho huo (gift deed). Hii husaidia kupunguza uwezekano wa migogoro ya baadaye.
    5. Pata Ushauri wa Kisheria: Wakili anaweza kukusaidia kuandaa nyaraka hizo kwa usahihi, kwa kuzingatia sheria, dini, au mila unayofuata, na kuhakikisha mchakato unaleta matokeo unayotamani kwa familia yako.

    Kumbuka: Kutopanga urithi kunaweza kusababisha mali zako kugawanywa kwa utaratibu wa kisheria ambao huenda hauakisi matakwa yako binafsi.

    Invictus Law and Consultancy tuko hapa kuhakikisha mipango yako ya urithi inatekelezwa kwa usahihi, kwa faraja na kwa mujibu wa sheria. Wasiliana nasi ili tukusaidie kuweka misingi imara ya ustawi wa familia yako.

  • Je, mtu akifariki bila kuacha wosia, mali zake hugawanywaje?

    Endapo mtu atafariki dunia bila kuacha wosia (hii huitwa intestate death), mgawanyo wa mali zake hufuata utaratibu wa sheria za mirathi za Tanzania, hasa Sheria ya Urithi ya Afrika Mashariki (The Probate and Administration of Estates Act), na mila au dini inayotumika, kulingana na mazingira ya familia husika.

    Kwa kawaida, hatua hizi hufuatwa:

    1. Kufungua Shauri la Mirathi Mahakamani: Ndugu wa karibu wa marehemu (mke/mume, mtoto, au jamaa wa damu) hufungua maombi ya kuwa msimamizi wa mirathi (administrator of estate) katika Mahakama ya Mwanzo au Mahakama Kuu kulingana na thamani ya mali.
    2. Uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi: Mahakama itateua mtu mmoja au zaidi kusimamia mali za marehemu na kuhakikisha zinagawanywa kwa warithi halali.
    3. Kutambua Warithi Halali: Mahakama itapokea ushahidi na kutambua warithi halali kulingana na sheria husika—ikiwa ni za kimila, Kiislamu, au sheria ya kiraia (statutory law).
    • Kwa Waislamu: Mgawanyo hufuata sheria ya Kiislamu ya urithi.
    • Kwa wengine: Mgawanyo unaweza kufuata mila au sheria ya kawaida kulingana na mwenendo wa maisha wa marehemu.

    4. Tathmini na Ugawaji wa Mali: Msimamizi wa mirathi atatathmini mali, kulipa madeni ya marehemu (kama yapo), kisha kugawa kilichobaki kwa warithi kulingana na uwiano ulioamriwa na sheria au mahakama.

    Muhimu: Hakuna mtu anayeruhusiwa kugawa mali ya marehemu kabla ya kupewa kibali rasmi cha kisheria na mahakama (probate or letters of administration). Kugawa mali kiholela ni kosa kisheria.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia katika kila hatua ya kufungua mirathi, kushughulikia migogoro kati ya warithi, na kuhakikisha haki za kila mrithi zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Tuwasiliane ili tukutafutie suluhu ya haraka na ya kisheria.

Masuala ya Ndoa, Talaka na Malezi ya Watoto

  • Je, nina haki ya kugawiwa mali tulizochuma pamoja hata kama mali hizo zimesajiliwa kwa jina la mwenza wangu?


    Ndio. Kisheria, mali yoyote iliyochumwa wakati wa ndoa—iwe imesajiliwa kwa jina la mume au mke—inaweza kuhesabiwa kuwa ni mali ya pamoja iwapo itathibitika kuwa ilichangiwa kwa namna yoyote na mwenza mwingine, iwe kwa pesa, kazi, au huduma za nyumbani.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania (Law of Marriage Act, Cap. 29 R.E. 2019) na tafsiri ya mahakama katika kesi mbalimbali (mfano: Bi Hawa Mohamed v. Ally Sefu), uchangiaji wa mali haupaswi kuwa wa kifedha pekee. Mchango wa kazi za nyumbani, malezi ya watoto, au kusaidia mwenza katika shughuli za kiuchumi unaweza kuhesabiwa kama mchango halali.

    Mahakama huzingatia mambo yafuatayo kugawa mali:

    Mchango wa kila mmoja katika ujenzi wa mali (wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja).

    Urefu wa ndoa.

    Mahitaji ya kila upande baada ya kuvunjika kwa ndoa.

    Uwezo wa kifedha wa kila upande.

    Kwa hivyo, jina la umiliki si kigezo pekee cha kuamua nani anamiliki mali. Ikiwa utathibitisha kuwa ulichangia kwa njia yoyote ile, unaweza kupata sehemu ya mali hizo wakati wa talaka au mgawanyo wa mali.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia kuthibitisha mchango wako na kudai haki yako ya mgawanyo wa mali kwa usahihi wa kisheria. Tunakutetea kwa weledi na maarifa ya ndani ya mfumo wa sheria za ndoa nchini Tanzania.

  • Je, ndoa ya kimila inatambulika kisheria?

    Ndio. Ndoa ya kimila inatambulika kisheria nchini Tanzania ikiwa itazingatia masharti ya kisheria na mila halali zinazokubalika na jamii husika.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act, Cap. 29 R.E. 2019), kifungu cha 9 na 11, ndoa ya kimila ni mojawapo ya aina nne za ndoa zinazotambulika kisheria (pamoja na ndoa ya kidini, ya kiraia, na ya ya mitala kwa mujibu wa mila).

    Masharti ya kutambulika kwa ndoa ya kimila ni pamoja na:

    1. Pande zote mbili kukubaliana kuingia kwenye ndoa.
    2. Ndoa kufungwa kulingana na taratibu za mila halali za jamii hiyo.
    3. Wanandoa wote wawili kuwa na umri wa kisheria (angalau miaka 18, au 15 kwa ruhusa ya mahakama).
    4. Kutoenda kinyume na sheria nyingine za nchi – kama vile kuoa wake zaidi ya mmoja bila ridhaa ya mke wa kwanza pale ambapo mfumo si wa mitala.

    Kwa nini ni muhimu kuthibitisha ndoa ya kimila?

    • Kuwezesha haki ya urithi, hasa kwa mke au watoto.
    • Kujilinda katika masuala ya talaka au mgawanyo wa mali.
    • Kuweza kusajili ndoa hiyo kwa hiari ili iwe rahisi kuthibitisha kisheria mbele ya vyombo vya sheria.

    Tafadhali kumbuka: Ikiwa ndoa ya kimila haijathibitishwa wala kusajiliwa, inaweza kuwa vigumu kuithibitisha mbele ya mahakama pale mzozo unapotokea.

    Invictus Law and Consultancy inakushauri kuwasiliana nasi iwapo umefunga au unapanga kufunga ndoa ya kimila ili tukuongoze katika hatua za kuisajili na kuitambua rasmi kwa mujibu wa sheria. Tunakupa mwongozo sahihi kwa kila hatua ya maisha ya kisheria ya ndoa.

  • Nifanye nini kama mume/mke hataki kutoa matunzo ya familia?

    Kisheria, mume na mke wana jukumu la kuhudumiana na kusaidiana kifamilia, ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, mavazi, matibabu na mahitaji ya watoto. Kukwepa jukumu hili ni kosa la kisheria.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania (Law of Marriage Act, Cap. 29 R.E. 2019), kifungu cha 63 na 129, kila mwenzi ana wajibu wa kuchangia mahitaji ya familia kwa kadiri ya uwezo wake.

    Hatua unazoweza kuchukua:

    1. Jaribu mazungumzo ya ndani ya familia.
    2. Wasiliana na Baraza la Usuluhishi la Ndoa katika eneo lako ili kupatiwa msaada wa kitaalamu wa mazungumzo ya usuluhishi.
    3. Fungua kesi mahakamani ya madai ya matunzo. Unaweza kuomba:
    • Amri ya matunzo kutoka kwa mume/mke kwa ajili ya familia au watoto.
    • Kiasi maalum cha pesa kulingana na uwezo wake na mahitaji ya familia.

    Ikiwa kuna dhuluma au kutelekezwa, unaweza pia kufungua kesi ya ndoa au hata ya jinai kutegemeana na mazingira.

    Matokeo ya kutokutoa matunzo:

    Mahakama inaweza kuamuru mshahara wa mume/mke ukatwe moja kwa moja au amri ya kukamatwa itolewe endapo hatatekeleza amri ya matunzo.

    Muhimu: Madai ya matunzo yanaweza kufunguliwa hata kama bado mnaishi pamoja, ilimradi upande mmoja ameshindwa kutimiza wajibu wake.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusaidia kufuatilia haki zako za kifamilia kwa utaratibu wa kisheria. Tunaelewa unavyohitaji msaada wa kisheria ulio thabiti. Wasiliana nasi kwa usaidizi wa kitaalamu.

  • Baada ya talaka, nani ana haki ya kuishi na Watoto wetu?

    Baada ya talaka, haki ya kuishi na watoto (custody) huamuliwa na mahakama kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto (best interest of the child), si kwa msingi wa jinsia au uwezo wa kifedha peke yake.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania (Law of Marriage Act, Cap. 29 R.E. 2019), kifungu cha 125 hadi 133, mahakama inaweza kumpa mzazi mmoja haki ya kuishi na watoto, na mwingine kupewa haki ya kuwaona au kutoa matunzo, kulingana na mazingira ya kesi.

    Mambo yanayoangaliwa na mahakama ni pamoja na:

    1. Umri wa mtoto: Watoto wenye umri mdogo (hasa chini ya miaka 7) mara nyingi hupewa mama isipokuwa kama kuna ushahidi wa wazi kuwa hilo halifai kwa ustawi wa mtoto.
    2. Uwezo wa mzazi kumlea mtoto: Hii ni pamoja na uwezo wa kimwili, kihisia na kimaadili.
    3. Mazoea ya mtoto: Mahakama huangalia pia mtoto amekuwa akiishi na nani kwa kipindi kirefu kabla ya mgogoro.
    4. Maoni ya mtoto: Ikiwa mtoto ana umri wa kuelewa (kawaida kuanzia miaka 10 na kuendelea), mahakama inaweza kuzingatia maoni yake.
    5. Tabia ya kila mzazi: Ikiwa mmoja amewahi kuwa na tabia mbaya kama manyanyaso, ulevi wa pombe au matumizi ya dawa za kulevya, inaweza kuwa sababu ya kukosa uangalizi wa moja kwa moja.

    Haki ya mzazi mwingine:

    Hata kama mzazi hatapewa uangalizi wa moja kwa moja, bado ana haki ya:

    1. Kumtembelea mtoto (access rights).
    2. Kutoa matunzo ya kifedha (maintenance).
    3. Kushiriki maamuzi muhimu ya maisha ya mtoto.

    Kumbuka: Uamuzi wa mahakama unaweza kubadilishwa baadaye ikiwa hali ya maisha au tabia za mzazi aliyekabidhiwa watoto zitabadilika.

    Invictus Law and Consultancy inatoa usaidizi wa kisheria katika masuala ya malezi ya watoto baada ya talaka, pamoja na usuluhishi wa haki za kila mzazi. Tunahakikisha maslahi ya mtoto yanazingatiwa kikamilifu huku tukikulinda kisheria. Wasiliana nasi kwa msaada wa kitaalamu na wenye utu.

  • Je, naweza kupata talaka hata kama mwenza wangu hataki kuachana?


    Ndiyo, kisheria unaweza kupata talaka hata kama mwenza wako hataki kuachana, endapo utathibitisha kuwa ndoa yenu imevunjika kiasi kwamba haiwezi tena kurekebishika.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act, Cap. 29 R.E. 2019), talaka hutolewa iwapo Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya au Hakimu Mkazi itaridhika kuwa kuna sababu za msingi zinazoonesha ndoa haiwezi tena kuendelea. Mambo yanayoweza kuthibitisha hali hiyo ni pamoja na:

    1. Usaliti wa mke au mume (adultery).
    2. Ukatili wa kimwili au kisaikolojia.
    3. Kutelekezwa kwa kipindi kisichopungua miaka miwili mfululizo.
    4. Kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, kama vile matunzo, mapenzi na heshima.
    5. Kufungwa gerezani kwa muda mrefu.
    6. Ugonjwa wa akili usioponyeka.

    Hatua zinazopaswa kufuatwa:

    1. Kwanza unapaswa kufungua malalamiko kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa lililoko kwenye eneo lako. Lengo ni kusaidia pande mbili kutafuta suluhu.
    2. Iwapo usuluhishi utashindikana, unaruhusiwa kufungua kesi ya talaka mahakamani.
    3. Mahakama itapokea ushahidi wako na ikiwa itaridhika kuwa ndoa imevunjika, itatoa amri ya talaka hata kama mwenza wako hataki.

    Muhimu: Kukataa kwa mwenza si kikwazo cha kisheria endapo ushahidi unaonesha ndoa imevunjika kimsingi.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kukusikiliza na kukushauri kwa kina kuhusu mchakato wa talaka, ikiwa ni pamoja na masuala ya malezi ya watoto na mgawanyo wa mali. Wasiliana nasi kwa msaada wa kisheria ulio salama, wa faragha na wenye weledi wa hali ya juu.

  • Je, nitalindwaje kisheria kama mwenza wangu ananisaliti au hanitii?

    Kisheria, usaliti katika ndoa (ugoni) na kutotekeleza majukumu ya ndoa kama vile upendo, heshima, uaminifu na matunzo, vinaweza kuwa msingi wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwenza.

    1. Kupitia Mahakama ya Mwanzo kwa Ushauri au Maelewano:

    Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act [Cap. 29 R.E. 2019]) inahimiza kwanza kutafuta suluhu kwa njia ya usuluhishi kupitia Baraza la Usuluhishi wa Ndoa (Marriage Conciliation Board). Unaweza kufungua malalamiko rasmi ukieleza tabia ya mwenza wako ya usaliti, manyanyaso, ama kushindwa kutekeleza majukumu ya kifamilia.

    2. Kutafuta Talaka kwa Sababu za Kisheria:

    Iwapo hali ni mbaya na haiwezi kurekebishika, unaweza kufungua kesi ya talaka kwa misingi ya:

    • Usaliti wa mume au mke (adultery).
    • Manyanyaso ya kimwili au kihisia.
    • Kutelekezwa kwa zaidi ya miaka miwili.
    • Kukosa majukumu ya kifamilia bila sababu ya msingi.

    3. Kuomba Amri Maalum kutoka Mahakamani:

    • Unaweza kuomba amri ya zuio dhidi ya mwenza anayeleta madhara.
    • Unaweza kuomba matunzo ya watoto au msaada wa kifedha (maintenance order).

    4. Kugawana Mali:

    Iwapo ndoa inavunjika kwa sababu ya usaliti au kutowajibika kwa mwenza, Mahakama inaweza kuagiza mgawanyo wa mali kwa kuzingatia mchango wa kila mmoja katika maisha ya ndoa, hata kama mali haikuandikwa kwa majina ya wote wawili.

    Kumbuka: Kwa mujibu wa kifungu cha 107 cha Sheria ya Ndoa, Mahakama huangalia mchango wa kila mwenza — wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja (kama ule wa nyumbani).

    Invictus Law and Consultancy ipo kwa ajili ya kukusaidia kujua haki zako na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Ikiwa unakabiliwa na matatizo ya usaliti au kutotimiziwa majukumu ndani ya ndoa, wasiliana nasi kwa ushauri wa kisheria wenye huruma na ufanisi.

Masuala ya Jinai na Polisi

  • Nifanye nini kama nimekamatwa bila sababu ya msingi?

    Kukamatwa bila sababu halali ni kinyume cha sheria na ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Endapo umekamatwa bila msingi wa kisheria, zipo hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kulinda haki zako:

    1. Omba kufikishwa mahakamani haraka

    • Kisheria unatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya masaa 24.
    • Ukiendelea kushikiliwa bila kufikishwa mahakamani, unaweza kuomba amri ya habeas corpus kupitia wakili wako ili ulazimishe kuletwa mbele ya jaji.

    2. Wasiliana na wakili mara moja

    • Wakili atakusaidia kuwasilisha malalamiko rasmi, kufuatilia dhamana, na kulinda haki zako wakati wa mahojiano.

    3. Toa taarifa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

    • Tume hii ina mamlaka ya kupokea na kuchunguza malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola.

    4. Fungua kesi ya madai ya fidia kwa kukamatwa kinyume cha sheria

    • Mahakama inaweza kuamuru fidia ya pesa kwa kukamatwa bila sababu au kushikiliwa kwa muda usio halali.

    5. Kumbukumbu sahihi

    • Hakikisha unaandika au kukumbuka jina la askari aliyekukamata, tarehe, muda, na eneo la tukio. Hii itasaidia katika ushahidi wa baadaye.

    Invictus Law and Consultancy tunakutetea dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka na kukamatwa kiholela. Wasiliana nasi kwa msaada wa haraka wa kisheria na ulinzi wa haki zako kila hatua ya safari ya kisheria.

  • Je, polisi wanaweza kunikamata bila hati ya kukamatwa?


    Ndio, polisi wanaweza kukamata mtu bila hati ya kukamatwa katika mazingira fulani yanayoruhusiwa na sheria, lakini sio kila wakati. Hii inategemea aina ya kosa linaloshukiwa na mazingira ya tukio.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20, polisi wanaweza kukamata bila hati ya kukamatwa kama:

    1. Kosa ni la jinai linaloadhibiwa kwa kifungo kisichopungua miaka mitatu au zaidi, kama vile wizi, ubakaji, au unyang’anyi.
    2. Mtu anakamatwa wakati akifanya kosa (caught in the act).
    3. Kuna hofu kwamba mtuhumiwa atatoroka au ataathiri upelelezi.
    4. Kuna sababu ya dharura na hakuna muda wa kupata hati kutoka kwa hakimu.

    Hata hivyo, hata kama kukamatwa ni bila hati:

    • Polisi wanapaswa kueleza sababu ya kukamatwa.
    • Mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya masaa 24.
    • Kukamatwa kusifanyike kwa kutumia nguvu isiyo ya lazima au kwa njia ya unyanyasaji.

    Ikiwa unahisi umekamatwa kinyume cha sheria au bila sababu halali, unaweza kuchukua hatua kupitia wakili au kwa kufungua malalamiko rasmi.

    Invictus Law and Consultancy iko tayari kusimama nawe kuhakikisha unapata haki yako, hasa katika mazingira nyeti kama haya. Wasiliana nasi kwa msaada wa kisheria wa haraka na madhubuti.

  • Je, ni haki zipi ninazo nikikamatwa na polisi?

    Kisheria, ukiwa umekamatwa na polisi, unaendelea kuwa na haki zako za msingi hadi ithibitishwe vinginevyo na mahakama. Haki hizi zinalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, pamoja na sheria mbalimbali za mwenendo wa jinai.

    Haki zako muhimu ni pamoja na:

    1. Haki ya kufahamishwa sababu ya kukamatwa kwa lugha unayoielewa (Kifungu cha 13(2) cha Katiba).
    2. Haki ya kukaa kimya ili usijipatie hatia.
    3. Haki ya kuwasiliana na wakili na kuwa na wakili wakati wa mahojiano.
    4. Haki ya kuwasiliana na ndugu au mtu unayemwamini.
    5. Haki ya kufikishwa mahakamani ndani ya masaa 24 tangu ukamatwe kama hakuna sababu halali ya kuchelewa (isipokuwa siku za mapumziko au likizo).
    6. Haki ya kutoteswa, kupigwa, au kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wakati wa upelelezi au mahojiano.
    7. Haki ya dhamana kwa makosa yanayodhaminika, isipokuwa kwa makosa makubwa yasiyodhaminika kama mauaji.

    Ikiwa haki hizi zitakiukwa, unaweza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.

    Invictus Law and Consultancy inakushauri usisite kuwasiliana nasi mara moja endapo utakamatwa au ndugu yako anakabiliwa na mchakato wa jinai. Tunatoa msaada wa haraka wa kisheria, kulinda haki zako tangu hatua ya kukamatwa hadi kesi kukamilika.