Na Wakili Steven Kitale Cleophace
Utangulizi
Katika ulimwengu wa utawala wa sheria, uwepo wa mfumo imara wa ulinzi wa mashahidi ni muhimu sana. Mashahidi ndio macho na masikio ya mahakama, na uwezo wao wa kutoa ushahidi bila hofu ni msingi wa kutendeka kwa haki. Ni katika muktadha huu ambapo Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, zilizotungwa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20), zinaonekana kuwa na nia njema ya kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu. Madhumuni makuu, kama yalivyobainishwa, ni kulinda mashahidi walio hatarini ili waweze kujitokeza na kutoa ushahidi, na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haki.
Hata hivyo, kama wakili ninayeshughulika na masuala ya haki jinai, nimechukua jukumu la kuchambua kwa kina vifungu vya kanuni hizi na Kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20 R.E. 2023). Uchambuzi huu unalenga kubaini iwapo utekelezaji wake unaweza kudhoofisha, au hata kukinzana na, haki za msingi za mshtakiwa zilizohakikishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan Ibara ya 13 (Haki ya Usawa Mbele ya Sheria) na Ibara ya 14 (Haki ya Kuishi). Kwani, haki hizi ni nguzo za mfumo wetu wa kisheria na zinahakikisha kila raia anapata fursa ya kusikilizwa kwa haki na kwa kufuata utaratibu halali wa kisheria.
Misingi ya Haki za Mshtakiwa Kikatiba
Kabla ya kuzama kwenye uchambuzi wa kanuni hizi, ni muhimu kukumbushana misingi ya haki za mshtakiwa kama ilivyowekwa na Katiba yetu adhimu:
Ibara ya 13(6)(a): Haki ya kusikilizwa kwa haki katika chombo chochote cha mahakama. Hii si tu haki ya kusikilizwa, bali ni haki ya kupata fursa ya kutosha na isiyo na vikwazo ya kujitetea.
Ibara ya 13(6)(b): Dhana ya kutokuwa na hatia mpaka itakapothibitishwa (presumption of innocence). Mshtakiwa huhesabika hana hatia hadi pale hatia yake itakapothibitishwa bila shaka na mahakama yenye mamlaka.
Ibara ya 15(2): Haki ya uhuru wa mtu, inayotafsiriwa kuwa inajumuisha haki ya utaratibu halali wa kisheria (due process of law), yaani, hakuna mtu anayepaswa kunyimwa uhuru wake isipokuwa kwa mujibu wa sheria na kwa kufuata taratibu stahiki.
Kutokana na misingi hii, haki ya kusikilizwa kwa haki inajumuisha mambo muhimu yafuatayo katika kesi za jinai:
Haki ya kukabili na kudodosha mashahidi wa upande wa mashtaka (right to confront and cross-examine witnesses). Hii inamaanisha kumwona shahidi, kusikia anachokisema, na kuwa na uwezo wa kumuhoji ili kubaini ukweli au udhaifu wa ushahidi huo.
Haki ya kupata taarifa kamili za mashtaka na ushahidi dhidi yake.
Haki ya kuwasilisha utetezi wake.Haki ya kusikilizwa mahakamani hadharani. Hii inahakikisha uwazi na uwajibikaji katika mfumo wa haki, isipokuwa kwa hali maalum.Haki ya kuwakilishwa na mwanasheria.
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi (2025) na Kifungu cha 194 cha CPA: Mwanga na Kivuli cha Haki
Pamoja na nia nzuri ya kulinda mashahidi, baadhi ya vifungu katika Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, pamoja na Kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20 R.E. 2023), vinaibua maswali makubwa kuhusu uhalali wake kikatiba na jinsi vinavyoathiri haki za mshtakiwa:
1. Maombi ya Upande Mmoja (Ex-Parte Application) – Kifungu cha 194(1) cha CPA na Kanuni ya 4(1)
Tatizo: Kifungu cha 194(1) cha CPA na Kanuni ya 4(1) zinampa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) pekee haki ya kuleta maombi ya ulinzi wa shahidi kwa njia ya ex-parte, yaani, bila mshtakiwa au wakili wake kuwepo au kusikia maombi hayo. Hii inamaanisha kuwa Mahakama inaweza kutoa amri muhimu zinazoathiri haki za mshtakiwa bila upande wa utetezi kupewa fursa ya kusikilizwa au kupinga.
Athari kwa Haki ya Mshtakiwa: Mshtakiwa ananyimwa haki yake ya kikatiba ya kusikilizwa kabla ya uamuzi muhimu unaoathiri haki zake kutolewa. Huu ni ukiukwaji wa msingi wa “audi alteram partem” (sikiliza upande wa pili), unaoambatana na haki ya kusikilizwa kwa haki.
Ukinzani na Katiba: Hali hii inakinzana waziwazi na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, ambayo inahakikisha kila mtu ana haki ya kusikilizwa kwa haki.
2. Kutofichua Utambulisho, Mahali, Kauli, na Nyaraka za Shahidi (Kifungu cha 194(1)(b) & (c), 194(2) cha CPA na Kanuni ya 3, 6(1)(a)(v), 6(1)(c)(ii))
Vifungu Husika:
CPA Kifungu cha 194(1)(b) & (c): Inaruhusu kutofichua au kuweka mipaka juu ya utambulisho au mahali alipo shahidi, na kutofichua kauli au nyaraka zinazoweza kusababisha utambulisho wa shahidi.
CPA Kifungu cha 194(2): Inasisitiza kuwa taarifa hizi hazitatolewa kwa mshtakiwa wakati wa uchunguzi wa awali (committal) au kesi.
Kanuni ya 6(1)(a)(v): Inaruhusu shahidi kutoa ushahidi “kwa kutumia vifaa vya kupotosha au kubadilisha picha au sauti, au akiwa haonekani.”
Kanuni ya 3: Inafafanua “kizimba maalum cha shahidi” kama sehemu iliyoundwa kumwezesha shahidi kutoa ushahidi “bila kuonekana isipokuwa kwa jaji au hakimu anayeendesha shauri husika.”
Athari kwa Haki ya Mshtakiwa: Haki ya mshtakiwa kumwona shahidi na kumuhoji ana kwa ana ni nguzo muhimu ya haki ya kusikilizwa kwa haki. Kutojua shahidi ni nani, au kutokuwa na uwezo wa kumwona au kujua mahali alipo, kunafanya iwe vigumu sana, au hata haiwezekani, kwa wakili wa utetezi kuhoji ushahidi kwa ufanisi. Mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, kama vile Ibara ya 14(3)(e) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, inasisitiza haki ya mshtakiwa kumhoji shahidi anayemshuhudia. Kutoona shahidi kunafanya haki hii kuwa tupu.
Ukinzani na Katiba: Hali hii inakinzana moja kwa moja na Ibara ya 13(6)(a) na Ibara ya 13(6)(b). Mshtakiwa hawezi kujitetea kwa ufanisi dhidi ya shahidi asiyejulikana, na dhana ya kutokuwa na hatia inakuwa batili wakati mshtakiwa ananyimwa zana muhimu za kuthibitisha kutokuwa na hatia yake.
3. Utoaji Ushahidi kwa Njia ya Video au Simu Bila Uwepo Halisi Mahakamani (Kifungu cha 194(1)(a) cha CPA na Kanuni ya 6(1)(b))
Vifungu Husika:
CPA Kifungu cha 194(1)(a): Inaruhusu ushahidi wa shahidi kutolewa kwa njia ya video (video conferencing) kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi.
Kanuni ya 6(1)(b): Inaruhusu utoaji wa ushahidi kupitia “mkutano kwa njia ya video akionekana kwa jaji au hakimu anayesikiliza shauri” au “mkutano kwa njia ya simu.”
Athari kwa Haki ya Mshtakiwa: Ingawa tunathamini maendeleo ya teknolojia, utoaji ushahidi kwa njia hizi unaweza kupunguza ufanisi wa kudodosha ushahidi ikilinganishwa na ushahidi wa ana kwa ana. Changamoto za kiufundi, ucheleweshaji wa sauti au picha, na ukosefu wa mawasiliano ya macho hupunguza uwezo wa wakili wa kupata ukweli kamili. Uwepo halisi wa shahidi mahakamani ni muhimu kwa mahakama na pande zote kutathmini usadikifu na uhalali wa ushahidi.
Ukinzani na Katiba: Matumizi ya kupita kiasi au yasiyo na udhibiti wa kutosha ya njia hizi, bila kuhakikisha fursa kamili ya kudodosha ushahidi, yanaweza kudhoofisha haki ya kusikilizwa kwa haki chini ya Ibara ya 13(6)(a).
4. Usikilizwaji wa Faragha (Kanuni ya 9(1) na (2))
Vifungu Husika: Kanuni ya 9(1) inampa mahakama mamlaka ya kuamuru shauri kusikilizwa faraghani kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kulinda shahidi, lakini pia ina kifungu kipana cha 9(1)(f) “sababu nyingine yoyote ambayo mahakama itaona inafaa.” Kanuni ya 9(2) inatoa uwezo wa kuwatenga watu wasio muhimu, hata wakati wa kusoma hukumu.
Athari kwa Haki ya Mshtakiwa: Haki ya kusikilizwa hadharani ni msingi wa uwazi na uwajibikaji katika mfumo wa haki. Kifungu cha “sababu nyingine yoyote inayofaa” ni pana sana na kinaweza kutumiwa vibaya, na hivyo kupunguza uwazi wa mahakama na kusababisha mashtaka kusikilizwa kwa siri isiyo ya lazima. Hii inapunguza imani ya umma katika mfumo wa haki na inapingana na dhana ya “haki haijifichi.”
Ukinzani na Katiba: Haki ya kusikilizwa kwa haki chini ya Ibara ya 13(6)(a), ingawa haitajwi waziwazi kuwa ni ya hadhara, kwa kawaida inatafsiriwa kujumuisha hadhara isipokuwa katika hali maalum na zenye msingi imara. Matumizi mapana ya faragha yanaweza kuifanya kanuni hii kuwa kinyume na matakwa ya kikatiba ya uwazi.
5. Wajibu wa Mahakama wa Kudhibiti Maswali (Kanuni ya 10(a) na Kifungu cha 194(1)(d))
Vifungu Husika:
Kanuni ya 10(a): Inampa jaji au hakimu anayesikiliza shauri uwezo wa “kudhibiti ipasavyo namna ya uulizwaji wa maswali kwa shahidi, ikiwa ni pamoja na kukataa swali ambalo linaloweza kupelekea kukiuka amri ya ulinzi au kusababisha bughudha, vitisho, hofu, au mkanganyiko kwa shahidi.”
CPA Kifungu cha 194(1)(d): Inaruhusu “hatua nyingine yoyote ya ulinzi ambayo mahakama inaweza kuona inafaa.” Kifungu hiki pana kinaweza kutumiwa kudhibiti maswali kwa njia isiyo ya haki.
Athari kwa Haki ya Mshtakiwa: Ingawa mahakama inawajibika kulinda shahidi dhidi ya unyanyasaji, vifungu hivi vinaweza kutumiwa vibaya kuzuia maswali muhimu na halali ambayo yangesaidia kubaini ukweli au udhaifu wa ushahidi wa shahidi. Hii inaweza kumnyima wakili wa utetezi uwezo wa kuchunguza ushahidi kwa kina, na hivyo kuvuruga kanuni ya usawa wa silaha (equality of arms) kati ya mashtaka na utetezi.
Ukinzani na Katiba: Kuzuia utetezi kudodosha ushahidi kwa kina, hata pale maswali yanapokuwa halali na yana lengo la kubaini ukweli, kunakiuka Ibara ya 13(6)(a). Haki ya kusikilizwa kwa haki inajumuisha haki ya kujitetea kwa ufanisi, na kudodosha ushahidi ni sehemu muhimu ya utetezi huo.
6. Mabadiliko ya Amri ya Ulinzi na Ukosefu wa Fursa kwa Mshtakiwa Kujitetea Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Mamlaka (Kanuni ya 8)
Kifungu Husika: Kanuni ya 8 inasema amri ya ulinzi inaweza kufutwa au kubadilishwa na mahakama “kwa utashi wake au kufuatia maombi” endapo kuna mabadiliko ya hali ya shahidi.
Jinsi Inavyodhoofisha Haki za Mshtakiwa: Kanuni hii haibainishi wazi kuwa mshtakiwa pia anaweza kuleta maombi ya kufuta au kubadilisha amri ya ulinzi. Ikizingatiwa Kanuni ya 4(1) inampa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pekee haki ya kuleta maombi ya awali ya ulinzi, kutokujumuishwa wazi kwa mshtakiwa katika Kanuni ya 8 kunamaanisha kuwa mshtakiwa hana haki sawa ya kushawishi mabadiliko ya amri.
Ukosefu wa Usawa wa Silaha na Ulinzi Dhidi ya Matumizi Mabaya: Hali hii inaleta ukosefu wa usawa wa silaha kati ya upande wa mashtaka na utetezi. Mshtakiwa ndiye anayeathirika moja kwa moja na amri ya ulinzi. Iwapo hali iliyosababisha amri hiyo kutolewa imebadilika (k.m., tishio limekwisha) au kama kuna hisia ya matumizi mabaya ya mamlaka kutoka upande wa mashtaka (DPP) au hata mahakama yenyewe (kwa kuendelea kutumia amri isiyo na msingi), mshtakiwa anapaswa kuwa na haki ya kuomba amri hiyo irekebishwe au ifutwe. Kukosekana kwa fursa hii kunamfanya mshtakiwa kuwa katika nafasi dhaifu na kumnyima utaratibu wa kisheria wa kupinga ukiukwaji wa haki zake.
Ukinzani na Katiba: Kukosekana kwa fursa kwa mshtakiwa kupinga au kuomba marekebisho ya amri ya ulinzi, hasa pale anapoona matumizi mabaya ya mamlaka au mazingira yamebadilika, kunanyima mshtakiwa fursa ya kutosha ya kujitetea na inakinzana na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba.
Kwa Nini Kanuni Hizi na Kifungu cha 194 Hazilindi Mashahidi wa Utetezi na Zipo Upande Mmoja Tu?
Hili ni hoja muhimu sana na linafichua mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni hizi na sheria mama. Kwa jinsi zilivyoundwa, zinaonekana kulenga kulinda mashahidi wa upande wa mashtaka pekee, na hivyo kuacha ombwe kubwa katika mfumo wa haki.
Tafsiri ya “Shahidi” (Kanuni ya 3): Ingawa tafsiri ya “shahidi” inasema “mtu anayehitaji ulinzi kutokana na tishio au hatari… kutokana na kutoa taarifa… au kutoa ushahidi kuhusiana na kosa au shauri la jinai,” tafsiri hii haibainishi wazi kama inajumuisha mashahidi wa utetezi. Kwa kawaida, kanuni zinapokuwa kimya au hazifafanui wazi, tafsiri inayoelekea upande mmoja ndiyo inayochukuliwa, na hapa inaonekana kuwa ni mashahidi wa DPP.
Maombi ya Amri ya Ulinzi (Kanuni ya 4(1) na Kifungu cha 194(1) cha CPA): Hapa ndipo tatizo linapoonekana wazi. Kanuni ya 4(1) na Kifungu cha 194(1) cha CPA zinasema wazi: “Mkurugenzi wa Mashtaka…anaweza kuleta maombi ya upande mmoja ya amri ya ulinzi wa shahidi.” Hakuna kifungu chochote kinachompa mshtakiwa au wakili wake haki ya kuleta maombi kama hayo kwa ajili ya mashahidi wa upande wa utetezi.
Athari ya Ukosefu wa Usawa:
Hatari kwa Mashahidi wa Utetezi: Mashahidi wa upande wa utetezi wanaweza kukabiliwa na vitisho au shinikizo kutoka kwa wahalifu, au hata kutoka kwa baadhi ya wadau wa Serikali, ili wasitoe ushahidi unaomuunga mkono mshtakiwa. Ikiwa kanuni hizi hazitoi utaratibu wa kuwalinda mashahidi hao, inamaanisha kwamba mashahidi muhimu wa utetezi wanaweza kuogopa kujitokeza, na hivyo kudhoofisha uwezo wa mshtakiwa kujitetea.
Ukosefu wa Usawa wa Silaha: Mfumo wa haki unapaswa kutoa usawa wa fursa kwa pande zote mbili. Ikiwa upande wa mashtaka unaweza kulinda mashahidi wake kwa urahisi, na upande wa utetezi hauwezi, inaharibu kanuni ya “usawa wa silaha” na kuweka mshtakiwa katika hali mbaya zaidi.
Kukinzana na Katiba (Ibara ya 13(6)(a) na (b)): Kukosekana kwa ulinzi kwa mashahidi wa utetezi kunanyima mshtakiwa fursa ya kutosha ya kujitetea na kuthibitisha kutokuwa na hatia yake. Hii inapingana na haki ya kusikilizwa kwa haki na dhana ya kutokuwa na hatia. Haki ya kujitetea inajumuisha haki ya kuita mashahidi na kuhakikisha wanaweza kutoa ushahidi wao bila hofu.
Hitimisho: Wito kwa Marekebisho ya Kikatiba na Usawa wa Kweli wa Sheria
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, pamoja na Kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20 R.E. 2023), ingawa zina lengo muhimu la kuimarisha utoaji haki, zina mapungufu makubwa yanayoweza kuzifanya ziwe kinyume na Katiba ya Tanzania na kudhoofisha usawa wa sheria. Zinaonyesha mwelekeo wa kulinda maslahi ya upande wa mashtaka kwa gharama ya haki za msingi za mshtakiwa.
Ni dhahiri kwamba: Haki za mshtakiwa kumkabili shahidi, kusikilizwa hadharani, na kudodosha ushahidi kikamilifu zinadhoofishwa.
Uwazi wa mchakato wa mahakama unahatarishwa.
Dhana ya kutokuwa na hatia inaminywa kwa sababu mshtakiwa ananyimwa fursa kamili ya kujitetea dhidi ya ushahidi usioonekana au usiohojiwa kikamilifu.
Na mbaya zaidi, Kanuni hizi na Kifungu cha 194 zinashindwa kutoa usawa kamili wa kisheria kwa mshtakiwa kupinga matumizi mabaya ya mamlaka au kulinda mashahidi wake mwenyewe, na hivyo kuziweka kanuni hizi upande mmoja tu wa Serikali (DPP na Mahakama).
Ukosefu huu wa usawa unavuruga kanuni ya usawa mbele ya sheria na haki ya mshtakiwa ya kupata mchakato halali wa kisheria. Kwa sababu hizi, naamini kuwa vifungu vilivyotajwa vinaweza kutafsiriwa kuwa kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa Ibara ya 13(6)(a) na Ibara ya 13(6)(b), na vinaweza kupingwa mahakamani. Ni muhimu kwa watunga sheria na mamlaka husika kuhakikisha kuwa sheria yoyote inayotungwa, hata kwa malengo mazuri, inazingatia na kuheshimu kikamilifu haki za msingi za binadamu kama zilivyohakikishwa na Katiba, kwa pande zote mbili katika shauri. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo tutaendelea kujenga mfumo wa haki ulio imara, wa uwazi, na unaotegemewa na wananchi wote.
Worth to read @Invictus #Home of Intellectual
Well elaborated sheria ya mashaidi na 194 CPA kwenye macho ya haki hazisimami
Umeeleweka vyema msomi
Given the compelling arguments you’ve made about the potential unconstitutionality and imbalance of the new Witness Protection Regulations and Section 194 of the CPA, particularly concerning the rights of the accused, what specific, actionable legislative amendments or judicial interpretations do you propose would effectively balance the legitimate need for witness protection against the fundamental constitutional rights to a fair hearing and an effective defense, without undermining either?
Proposed Legislative Amendments
1. Amendments to Ex-Parte Applications (Section 194(1) CPA and Regulation 4(1))
Proposed Amendment: Amend Section 194(1) of the CPA and Regulation 4(1) to require that applications for witness protection orders, while still potentially initiated ex parte in urgent cases, must be subject to an immediate or very swift inter partes hearing (with both sides present) once the initial protective measures are in place. The accused or their counsel should be given an opportunity to be heard and challenge the necessity and scope of the protection order.
Rationale: This maintains the ability to provide immediate protection while upholding the constitutional right to be heard. The ex parte nature should be a temporary measure, not a permanent exclusion of the defense.
2. Safeguarding the Right to Confront and Cross-Examine (Section 194(1)(b) & (c), 194(2) CPA and Regulations 3, 6(1)(a)(v), 6(1)(c)(ii))
Proposed Amendment: Introduce provisions that explicitly define the exceptional circumstances under which a witness’s identity or location can be withheld, and when testimony can be given without direct visual contact. These circumstances should be narrowly construed and demonstrably proven by the prosecution to a high standard (e.g., real and imminent threat to life or severe bodily harm that cannot be mitigated by less restrictive means).
Proposed Amendment: Mandate that even when identity is withheld, the defense must be provided with sufficient background information about the witness (e.g., their criminal record, any prior inconsistent statements, or potential biases) to effectively cross-examine them without revealing their identity.
Proposed Amendment: Regarding the use of image/voice distortion or special witness boxes, amend Regulation 6(1)(a)(v) and Regulation 3 to require that the court ensures the distortion does not impede the defense’s ability to assess the witness’s demeanor and credibility. The judge should have the discretion to order clearer visuals or audio if the distortion is excessive.
Rationale: These amendments aim to strike a balance between protecting witnesses and ensuring the accused can still effectively challenge the evidence against them, a cornerstone of a fair trial. The ability to assess demeanor is crucial for credibility.
3. Regulating Video and Telephone Testimony (Section 194(1)(a) CPA and Regulation 6(1)(b))
Proposed Amendment: Amend Section 194(1)(a) of the CPA and Regulation 6(1)(b) to stipulate clear conditions and technical standards for remote testimony. The court must be satisfied that the technology allows for effective real-time cross-examination, free from significant technical delays or disruptions.
Proposed Amendment: The use of remote testimony should be reserved for genuinely exceptional circumstances, such as witnesses located abroad, those with severe disabilities preventing court attendance, or those facing a proven, immediate threat that cannot be mitigated otherwise. It should not become the norm.
Rationale: While technology can facilitate justice, it should not compromise the quality of evidence or the defense’s ability to thoroughly test it.
4. Limiting Private Hearings (Regulation 9(1) and (2))
Proposed Amendment: Amend Regulation 9(1)(f) to remove the broad “any other reason the court deems appropriate” clause for private hearings. Instead, provide a closed list of specific, justifiable reasons for private hearings, such as national security cases, matters involving minors, or highly sensitive commercial secrets, ensuring these are narrowly defined.
Proposed Amendment: Regulation 9(2) should be amended to explicitly state that the pronouncement of judgment must always be in open court, unless there are exceptional, clearly defined circumstances that are strictly necessary to protect specific, identifiable individuals from grave and immediate harm.
Rationale: Public trials are fundamental to judicial transparency and accountability. Exceptions should be rare and clearly justified to prevent abuse and maintain public trust.
5. Balancing Judicial Control Over Questions (Regulation 10(a) and Section 194(1)(d))
Proposed Amendment: Amend Regulation 10(a) to clarify that while the court can control the manner of questioning, it cannot disallow questions that are relevant and aimed at eliciting truth or testing credibility, even if they might cause discomfort to the witness, unless such questions are clearly harassing, abusive, or designed solely to expose protected information unnecessarily.
Proposed Amendment: Add a proviso that the court, when exercising its discretion under Section 194(1)(d), must provide clear reasons on record for disallowing any question, demonstrating how it would specifically violate a protection order or cause undue harm, and ensuring it does not infringe on the right to an effective defense.
Rationale: This aims to prevent the misuse of protective measures to shield witnesses from legitimate scrutiny, preserving the “equality of arms” principle.
6. Ensuring Defense’s Right to Challenge Protection Orders (Regulation 8)
Proposed Amendment: Amend Regulation 8 to explicitly grant the accused or their counsel the right to apply to the court to vary or rescind a witness protection order. This application should be based on a change in circumstances (e.g., threat has ceased) or an assertion of abuse of process.
Proposed Amendment: Furthermore, Regulation 8 should state that the court, when considering such an application, must hold an inter partes hearing and provide detailed reasons for its decision.
Rationale: This addresses the current imbalance where only the DPP can initiate applications for protection orders. The defense, being directly affected, must have an equal right to seek review or modification of these orders when circumstances warrant.
7. Extending Protection to Defense Witnesses
Proposed Amendment: Amend the definition of “witness” in Regulation 3 and specifically amend Regulation 4(1) and Section 194(1) of the CPA to explicitly include provisions for the defense to apply for witness protection orders for their own witnesses.
Rationale: This is perhaps the most crucial amendment to ensure genuine “equality of arms.” If defense witnesses face threats, they too should have access to protection mechanisms, otherwise, the accused’s right to present a full defense is severely undermined.
Proposed Judicial Interpretations:
In the absence of immediate legislative amendments, courts can, and should, adopt interpretations that align with constitutional principles:
1. Strict Scrutiny of Witness Protection Applications
Interpretation: Courts should interpret the provisions related to witness protection with strict scrutiny, placing a high burden on the prosecution to demonstrate the absolute necessity of each requested protective measure. This means requiring concrete evidence of a genuine threat, not mere speculative fear.
Rationale: This ensures that protective measures are only granted when truly essential and proportionate to the threat, minimizing the impact on the accused’s rights.
2. Prioritizing the Right to Confrontation
Interpretation: Judges should prioritize the accused’s constitutional right to confront and cross-examine witnesses, interpreting any restrictions on this right very narrowly. Where possible, judges should seek alternative protective measures that have the least restrictive impact on this right.
Rationale: The right to confront one’s accuser is fundamental to a fair trial and should only be derogated from in the most compelling circumstances.
3. Ensuring Effective Cross-Examination with Remote Testimony
Interpretation: When remote testimony is allowed, judges must actively ensure the technical quality of the connection and the ability of both the defense and the court to observe the witness’s demeanor. If technical issues impede effective cross-examination, the judge should have the discretion to adjourn or even disallow such testimony.
Rationale: Technology should serve justice, not hinder it.
4. Promoting Transparency in Proceedings
Interpretation: Courts should interpret the provisions for private hearings in light of the principle of open justice. Any decision to hold a private hearing or exclude the public should be accompanied by clear, detailed, and publicly stated reasons, demonstrating the exceptional nature and necessity.
Rationale: Transparency builds public confidence in the judicial system.
By implementing these legislative amendments and encouraging robust judicial interpretations, Tanzania can build a witness protection framework that is both effective in combating crime and, crucially, fully compliant with its constitutional commitment to a fair and just criminal justice system for all.